Ushirika wa Udiakonia Faraja
UMOJA WA UNDUGU WA WADIAKONIA.
Ushirika wa Diakonia Faraja ni Umoja wa Undugu wa Wadiakonia wa kiume na unamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini. Wadiakonia ni watu wenye wito wa kweli na walioelimishwa na kubarikiwa kuwa watumishi katika huduma ya Diakonia katika Kanisa na jamii kwa ujumla. Kituo chetu kipo karibu na mji mdogo wa Sanya Juu, Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro. Kwenye kituo hiki ndipo yalipo makao makuu ya Umoja wa Wadiakonia wote wa Dayosisi ya Kaskazini na ndipo mahali yanapotolewa mafunzo ya Udiakonia.
WADIAKONIA WANATUMIKA WAPI KATIKA KANISA.
Wadiakonia wanaweza kufanya kazi Sharikani, kwenye majimbo ya Dayosisi zetu na kwenye vituo vya Kanisa vinavyotoa huduma za Diakonia au vinavyohitaji taaluma aliyonayo Mdiakonia. Kwa kuwa na elimu ya Sekondari, mafunzo ya Udiakonia na elimu katika taaluma nyingine atakayokuwa nayo. Mdiakonia anaweza kufanyakazi kwenye vituo mbali mbali vya Kanisa mfano:Kuratibu huduma ya Diakonia ngazi ya jimbo katika Dayosisi zetu, Mdiakonia mwenye taaluma ya ualimu anaweza kufanyakazi katika shule za Kanisa kama mwalimu au Mkuu wa shule, Kama mratibu au msimamizi wa miradi ya Kanisa inayowahudumia Yatima , walemavu wa viungo, au walemavu wa akili, Watakaokuwa na taaluma ya afya ya binadamu wanaweza kufanyakazi katika vituo vya afya au hospitali za Kanisa, na watakaokuwa na taaluma ya uhasibu wanaweza kufanyakazi kama Wahasibu katika vituo mbali mbali vya Kanisa.
Our Mission
Mission Statement
To provide comprehensive care for people in mental, social or physical need, train young men to become Deacons of the ELCT/ND in order to enable them to support people in a professional way. To increase land for development of centers that trains young men to become Deacons and also establish economic projects for sustainability of the developed center; and provide Primary School Education for Physical handicapped children.
Our Vision
Vision Statement
To be Gods servants, who serve the Society, according to Christ’s words and deed, by providing good diaconal service in Tanzania.
Matangazo News
Marafiki zetu
- Rummelsberg
Shirika la wadiakonia pale Ujerumani - KKKT
Dayosisi 25 za kanisa la kinjili la kilutheri Tanzania - KKKT Dayosisi ya Kaskazini
Makao Makuu ya Dayosisi yetu - Stefano Moshi Memorial University College
High Instution own by the Northern Diocese - Kiumo Mwika
Vocation Training run by the Parish in ND - Uhuru Hotel
Center for the Conference and place for the Retreat