Ujumbe wa Mkuu wa kanisa na Mkuu wa dayosisi Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo

Tunamshukuru Mungu kwa kuliwezesha Kanisa kuwa na Huduma ya Udiakonia na kuanzishwa kwa Ushirika wa Diakonia Faraja ambako wadiakonia huandaliwa na kutumika katika Dayosisi ya Kaskazini na kanisa kwa ujumla.

Tumebarikiwa na huduma hii hasa kwa kuona watu wanapokea upendo wa Mungu katika huduma mbalimbali wanazotoa kwa jamii yetu. Sisi Kanisa tunazidi kumuomba Mungu mwenyewe aendelee kuutunza na kuukuza Ushirika wa Diakonia Faraja kwa kuwaleta vijana wenye wito wa kweli kutoka pande zote za nchi.

Ujumbe wa Kaka Mkuu Ushirika wa Diakonia Faraja

Ushirika wa Udiakonia Faraja ni Umoja wa wandugu uko chini ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini ambao ni wanaume, vijana wenye wito wa kweli katika kumtumikia Kristo hujiunga nao.

Wadiakonia 28 hadi sasa wako katika vituo wakifanya kazi. Wadiakonia wanafanya kazi mbalimbali katika idara tofauti tofauti za kanisa na wengine za serikali zikiwa zinatoa huduma katika jamii ya kitanzania.

Kwa sasa Ushirika uko na wanafunzi 25, wako katika ngazi tofauti ambao wengine wako mwaka wa tano na pia wanafanya kazi katika jamii na wengine masomoni na mazoezi na wale ambao wapo kwenye kozi ya Msingi ndani ya ushirika na kujifunza kozi ya udiakonia theolojia na ustawi wa jamii.

Ushirika wetu wa Udiakonia unapenda sana kuwaambia vijana wenye wito kuja kujiunga na ushirika ili kuweza kulijenga kanisa. Kanisa letu la kilutheri huwa linatoa huduma ya neno na matendo hasa kwa wahitaji ambao ushirika wa udiakonia unalengo la kutoa huduma kwa matendo kuliko neno na hasa kwa kuangalia Matendo ya Mitume 6:1-7.

Image Gallery

Services Overview

Ushirika wa Udiakonia Faraja Tunatoa huduma mbalimbali katika jamii ambayo imetuzunguka na kwa kanisa hasa kwa wale ambao walikuwa wamesahaulika katika jamii, Ndio maana tulianzisha shule ya msingi kwa watoto wenye ulemavu wa viungo.

Contact Us

Unaweza kutufikia kwa mawasiliano haya au kufika sanya juu mjini na kupanda Noah za karansi na kushuka kwa Mapadre.

Address: P.O.Box 167, Sanya Juu
Telephone: +255 755 807 199
Mobile: +255 766 515 319
Mobile: +255 757 618 508
E-mail: info@ushirika-wa-udiakonia-faraja.org

Imetengenezwa na Ushirika wa Udiakonia Faraja