Tunamshukuru Mungu kwa kuliwezesha Kanisa kuwa na Huduma ya Udiakonia na kuanzishwa kwa Ushirika wa Diakonia Faraja ambako wadiakonia huandaliwa na kutumika katika Dayosisi ya Kaskazini na kanisa kwa ujumla.
Tumebarikiwa na huduma hii hasa kwa kuona watu wanapokea upendo wa Mungu katika huduma mbalimbali wanazotoa kwa jamii yetu. Sisi Kanisa tunazidi kumuomba Mungu mwenyewe aendelee kuutunza na kuukuza Ushirika wa Diakonia Faraja kwa kuwaleta vijana wenye wito wa kweli kutoka pande zote za nchi.